Shirika la hifadhi za taifa Tanzania laanzisha utalii wa baiskeli kwenye Mlima Meru
2022-05-09 08:22:59| CRI

Shirika la hifadhili za taifa Tanzania (TANAPA) jana jumapili lilizindua utalii wa kutumia baiskeli wakati wapanda baiskeli 27 walianza kupanda Mlima Meru wenye mwinuko wa mita 4,566.

Wapanda baiskeli hao 27, wakiwemo watalii na waongozaji wao, walianza jaribio lao la kufika kwenye kilele cha Mlima Meru ambacho ni cha tano barani Afrika, safari ambayo itawachukua siku tatu kupanda na kushuka.

Akiongea chini ya Mlima Meru, kamishina msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha Bw. Albert Mziray, amesema utalii wa kutumia baiskeli kwenye mlima ni dhana mpya yenye mustakbali wa kuvutia watalii wengi zaidi kwenye eneo hilo.