Rais Xi Jinping kuhutubia mkutano wa maadhimisho ya miaka 100 ya Umoja wa vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China
2022-05-09 08:20:07| CRI

Rais Xi Jinping wa China anatazamiwa kuhudhuria na kuhutubia mkutano wa maadhimisho ya miaka 100 ya Umoja wa vijana wa Chama cha kikomunisti cha China, utakaofanyika kesho kwenye Jumba la mikutano ya umma la Beijing.

Tukio hilo litatangazwa moja kwa moja na vyombo vikubwa vya habari vya China, ikiwa ni pamoja na tovuti za vyombo vya habari vya serikali na app za habari.