Jeshi la Iraq lawaua wapiganaji wa kundi la IS, na kuwakamata viongozi wake
2022-05-09 08:26:40| CRI

Jeshi la Iraq limesema limewaua wapiganaji watatu wa kundi la Islamic State (IS) na kuwakamata viongozi watatu wa kundi hilo katika majimbo ya Nineveh na Baghdad.

Jeshi la Iraq lilifanya operesheni katika eneo la milimani la mkoa wa kaskazini wa Ninawi na kuwaua wanamgambo watatu wa kundi hilo. Ofisi ya habari ya Kamandi ya Operesheni ya Pamoja (JOC) imesema kufuatia habari za kijasusi walizopata kutoka kwa wapiganaji waliokamatwa, waliweza kuwakamata viongozi wa kundi la IS wa eneo la Baghdad.

Hali ya usalama nchini Iraq inaendelea kuboreshwa tangu kundi la IS liliposhindwa mwaka 2017, hata hivyo mabaki ya wapiganaji wa kundi hilo wanaendelea kufanya mashambulizi ya kushitukiza dhidi ya vikosi vya usalama na raia.