China yatoa wito wa ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na ukame na kuzuia ardhi kugeuka kuwa jangwa
2022-05-10 09:11:45| CRI

Waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na ukame na kuzuia ardhi kugeuka kuwa jangwa.

Bw. Wang Yi akiwa ni mwakilishi maalumu wa Rais Xi Jinping, alitoa kauli hiyo kwa njia ya video kwenye mkutano mmoja wa viongozi kuhusu ukame na usimamizi endelevu wa ardhi.

Bw. Wang Yi amependekeza kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kuhimiza maendeleo ya kijani, na kuboresha kanuni za kimataifa juu ya kukabiliana na ukame na jangwa, ili kutatua changamoto hizo zinazoikabili jumuiya ya kimataifa.