China yarusha chombo cha kusafirisha mizigo kwenye kituo chake cha anga ya juu
2022-05-10 09:11:04| CRI

China imerusha chombo cha anga ya juu cha Tianzhou-4 ili kupeleka mahitaji kwenye kituo chake cha anga ya juu ambacho ujenzi wake umepangwa kukamilika mwaka huu.

Kwa mujibu wa Shirika la Anga ya juu la China CMSA, chombo cha Tianzhou-4 kilirushwa kwa kutumia roketi ya Long March-7 Y5 kutoka kwenye kituo cha kurushia vyombo vya anga ya juu cha Wenchang, mkoani Hainan.

Chombo hicho kimebeba mahitaji yanavyowatosheleza wanaanga kuishi angani kwa miezi sita, vipuri vya kituo cha anga na vifaa vya utafiti.