China yasaidia Namibia kuimarisha nafasi yake ya kikanda kwa ujenzi wa miundombiunu
2022-05-10 09:32:03| CRI

Sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa kuboresha barabara ya Windhoek hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako ilifanyika jana huko Windhoek, Nambia.

Waziri wa ujenzi na uchukuzi wa Namibia Bw. John Mutorwa alieleza kwenye sherehe hiyo kwamba mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya China unajumuisha ujenzi wa barabara kuu yenye urefu wa kilomita 21.3, madaraja matatu yanayopita juu ya barabara, madaraja mawili ya mito na mifereji ya maji. Mradi huo utaisaidia Namibia kupanua mtandao wake wa barabara wakati inafanya juhudi kutimiza malengo ya Dira ya 2030 katika sekta ya uchukuzi.

Konsela mkuu wa ubalozi wa China nchini Namibia Bw. Yang Jun amesema mradi huo uliopendekezwa na serikali ya Namibia na kuungwa mkono na ubalozi wa China, una lengo la kuisaidia Namibia kuwa kitovu cha uchukuzi kusini mwa nchi Afrika.

Mradi huo unaotarajiwa kumalizika baada ya miezi 36, utaleta ajira zaidi ya 300 kwa wenyeji na kuhimiza uhamishaji wa ujuzi wa teknolojia.