Rais Xi Jinping azungumza na mwenzake wa Ufaransa kwa njia ya simu
2022-05-11 08:32:14| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Kwenye mazungumzo yao, rais Xi ametaja mawasiliano ya karibu kati yake na rais Macron katika miaka mitano iliyopita, ambayo yamesaidia kuziongoza nchi hizo mbili kudumisha mwelekeo wa uhusiano wa pande mbili, kuendeleza ushirikiano na kutekeleza majukumu ya nchi kubwa kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi, uhifadhi wa bioanuwai na mengineyo.

Rais Xi amesema, China na Ufaransa, zikiwa ni wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zinapaswa kushikilia “uhuru, maelewano, maono ya kimkakati na ushirikiano wa kunufaishana” kama ilivyoahidiwa na pande hizo mbili zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia, kushikilia uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili, kuheshimu maslahi makuu na ufuatiliaji mkubwa wa upande mwingine, na kuimarisha uratibu na ushirikiano kati ya pande mbili, kati ya China na Ulaya na kwenye mazingira ya kimataifa.