Ofisa wa UNICEF atoa wito kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wasichana kaskazini mwa Nigeria
2022-05-12 08:49:00| CRI

Ofisa wa Shirika la Kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Bw. Rahama Faraha, ametoa wito kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wasichana kaskazini mwa Nigeria, ambako kuna idadi kubwa ya wasichana wasiokwenda shule.

Bw. Faraha amesema hivi sasa kuna watoto milioni 18.5 wasiokwenda shule nchini Nigeria, takriban asilimia 60 kati yao wakiwa wasichana. Hali hii inaongeza ukosefu wa usawa wa kijinsia, ambapo ni msichana mmoja tu kati ya wanne kutoka familia maskini za vijijini, anaweza kuhitimu elimu ya sekondari.

Mashambulizi yanayofanywa na watu wenye silaha dhidi ya shule katika sehemu za nchi hiyo, yamesababisha kudorora kwa hali ya upatikanaji wa elimu kwa wasichana.