Jeshi la Ujerumani kuendelea na operesheni za UM nchini Mali
2022-05-12 08:30:38| CRI

Serikali ya Ujerumani imesema jeshi la nchi hiyo litaendelea kuiunga mkono Tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda utulivu nchini Mali (MINUSMA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatano, ushiriki wa jeshi la Ujerumani katika tume hiyo ulioanza mwaka 2013, utarefushwa hadi mwisho wa Mei mwaka 2023.

Taarifa hiyo inasema upangaji wa vikosi vya Ujerumani utategemea maendeleo ya hali ya kisiasa nchini Mali, matokeo ya uamuzi wa Ufaransa kuondoa jeshi lake, na “mahitaji ya ziada ya vikosi” kwenye upande wa mashariki wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi, NATO.