Ndege yenye watu 11 iliyopoteza mawasiliano nchini Cameroon yapatikana kwenye misitu
2022-05-12 08:45:45| CRI

Waziri wa uchukuzi wa Cameroon Bw. Ernest Bibehe amesema ndege iliyokuwa na watu 11 na kupoteza mawasiliano, imepatikana kwenye eneo moja la misitu karibu na mkoa wa kati.

Ndege hiyo iliruka kutoka mji wa Yaoundé ikielekea katika mji wa Mashariki wa Belabo ikiwa na wafanyakazi wa kampuni ya mafuta.

Timu ya uokoaji inaelekea kwenye eneo ilipo ndege hiyo ili kutoa msaada kwa watu waliokuwa kwenye ndege hiyo.