Ubalozi wa China wazindua mpango wa vyombo vya habari ili kuhimiza amani nchini Sudan Kusini
2022-05-13 08:37:57| CRI

Umoja wa Wanahabari wa Sudan Kusini na ubalozi wa China nchini humo jana Alhamisi walizindua kwa pamoja mpango wa utoaji ripoti wa “My Peace” unaolenga kusambaza taarifa za amani na kuhamasisha ushiriki wa umma, wakiungwa mkono na Wizara ya Ujenzi wa Amani ya Sudan Kusini.

Waziri wa Ujenzi wa Amani Bw. Stephen Par Kuol, amesema kuna haja ya kutoa ripoti chanya kuhusu Sudan Kusini baada ya vurugu za miaka mingi kumalizika kufuatia kusainiwa kwa makubaliano ya amani ya mwaka 2018.

Balozi wa China nchini Sudan Kusini Hua Ning amesema Sudan Kusini ambayo ni nchi changa zaidi duniani, imeshuhudia maendeleo chanya katika mchakato wa amani, hali ambayo imehimiza ufufukaji wa uchumi.