Haki za Wanawake wanapotengana na wenzi wao
2022-05-13 08:59:18| CRI

Suala la ndoa na talaka limekuwa likijadiliwa mara kwa mara, na jambo hili linaleta utata mkubwa maana pindi wanadoa wanapotengana, mgogoro mkubwa kuhusu kugawana mali hutokea. Lakini je, ni mali pekee ambayo inapaswa mwanamke kufidiwa? Vipi kuhusu muda wake alioutumia katika kutunza familia? 

Katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake siku ya leo tutaangalia suala hili la talaka na haki za mwanamke pindi anapoachana na mume wake.