Mshambuliaji mzungu akamatwa saa chache baada ya shambulizi
2022-05-16 08:42:12| CRI

Mwanaume mmoja mzungu mwenye umri wa miaka 18 aliyetambuliwa kwa jina la Payton Gendron, amekamatwa usiku wa Jumamosi, saa kadhaa baada ya kufanya shambulizi la risasi katika duka moja kubwa mjini Buffalo, Marekani, ambalo alilirekodi moja kwa moja.

Kijana huyo aliyekuwa na silaha nzito alijisamilisha katika kituo cha polisi cha mji huo baada ya kuua watu 10 na kujeruhi wengine watatu Jumamosi mchana katika duka hilo.

Ripoti zinasema, mshambuliaji huyo alirekodi shambulizi lake kupitia jukwaa la Twitch, na kuandika ujumbe unaohusiana na ubaguzi wa rangi.