Raila Odinga amteua Martha Karua kuwa mgombea mwenza.
2022-05-16 19:25:40| cri


Aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amemteua Martha Karua kuwa mgombea wake mwenza katika uchaguzi mkuu wa Agosti tisa.

Ni kwanza Kenya kwa mgombea maarufu wa urais kumteua mgombea mwenza mwanamke.

Martha Karua pia atahudumu kama waziri wa haki, sheria na katiba ikiwa muuungano wao wa azimio utatwaa ushindi.

Uteuzi huu umepokelewa kwa shangwe na wanawake nchini Kenya.

Karua aliwahi kuwa waziri wa maji na sheria katika serikali za awali na sasa anaongoza chama cha Narc Kenya.

Jumapili naibu wa Rais nchini humo William Ruto alimteua mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua kuwa mgombea mwenza wake.

Uchaguzi huo umevutia wagombea kadhaa lakini ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya Raila na Ruto.