Chama tawala nchini Sweden kuunga mkono ombi la nchi hiyo kujiunga na NATO
2022-05-16 08:44:54| CRI

Chama tawala nchini Sweden (SAP) kimeridhia na kuunga mkono ombi la nchi hiyo kujiunga na Jumuiya ya NATO, na kuweka alama muhimu ya mabadiliko ya nafasi ya chama kama mpinga thabiti wa ushirikiano wa kijeshi.

Akizungumza na wanahabari jana, waziri mkuu wa nchi hiyo Magdalena Anderson ambaye pia ni kiongozi wa Chama hicho amesema, wanaamini kuwa kitu muhimu kwa usalama wa Sweden ni kujiunga na NATO.

Mabadiliko ya msimamo wa SAP kuhusu NATO yanachukuliwa kuwa ya kihistoria, kwa kuwa siasa za chama hicho zinaweka wazi kuwa uhuru wa uhusiano wa kijeshi ni msingi wa sera ya usalama ya Sweden.

Hata hivyo, uamuzi huo umekosolewa vikali na upande wa upinzani nchini humo ambao unasema hatua hiyo inaweza kuipeleka Sweden na dunia kwa ujumla kwenye mwelekeo usio sahihi.