Umoja wa Ulaya wapunguza makadirio ya ongezeko la uchumi
2022-05-17 09:05:26| CRI

Ripoti ya makadirio ya uchumi ya majira ya mchipuko ya mwaka 2022 iliyotolewa na Kamati ya Umoja wa Ulaya imesema, kutokana na mgogoro kati ya Russia na Ukraine, kamati hiyo imepunguza makadirio ya ongezeko la uchumi wa Umoja huo kwa mwaka huu na mwaka ujao.

Ripoti hiyo inakadiria kuwa, uchumi wa Umoja wa Ulaya unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 2.7 na asilimia 2.3 mwaka 2022 na mwaka 2023, kiasi ambacho kiko chini ya asilimia 4 na asilimia 2.8 zilizokadiriwa katika ripoti ya majira ya baridi iliyotolewa mwezi Februari mwaka huu.

Mjumbe wa Kamati hiyo anayeshughulikia mambo ya uchumi Bw. Paolo Gentiloni amesema, mgogoro kati ya Russia na Ukraine umeathiri vibaya uchumi, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa kasi kwa bei za bidhaa za matumizi, na kuongezeka kwa ukosefu wa utaratibu wa mnyonyoro wa ugavi wa bidhaa.