Wanajeshi wa Somalia na Umoja wa Afrika wakamata tena kambi ya kijeshi kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabab
2022-05-18 08:45:30| CRI

Wanajeshi wa Tume ya mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) na jeshi la Somalia (SNA) jana wamekamata tena kambi ya kijeshi ya El-Baraf kwenye eneo la Shabelle ya Kati, Kusini Magharibi mwa Somalia, wiki mbili baada ya wapiganaji wa al-Shabab kuikamata kutoka kwa vikosi vya Burundi.

Kamanda wa jeshi la Somalia anayeongoza operesheni hiyo Tabane Ahmed Gurey amesema vikosi vya pamoja vimedhibiti kambi hiyo.

Mei 3, wapiganaji wa al-Shabab walikalia kambi hiyo ya vikosi vya Burundi iliyo chini ya kambi ya kijeshi ya Umoja wa Afrika, na kutangaza kuwa wamewaua askari 173 na kuwakamata wengine kadhaa.