Russia yasema Ukraine imejitoa kihalisi kwenye mchakato wa mazungumo kati ya nchi hizo mbili
2022-05-18 08:42:12| cri


 

     Shirika la habari la Russia RIA Novosti limemnukuu waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergey Lavrov akisema, Ukraine imejitoa kihalisi kwenye mchakato wa mazungumzo kati yake na Russia, huku mshauri wa ofisi ya rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak akisema, mchakato wa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili umesitishwa.

    Bw. Lavrov amesema, wawakilishi wa Ukraine wanaelekezwa na Marekani na Uingereza, na kwamba nchi za Magharibi zinataka kuchelewesha mazungumzo kati ya Russia na Ukraine, ili kuiletea hasara Russia na kuiangusha. Amesema Russia ina ushahidi kuwa nchi za Magharibi hazina mpango wa kutoa uhakikisho wa usalama kwa Ukraine.