Serikali ya mpito ya Mali yazuia jaribio la mapinduzi ya kijeshi
2022-05-18 09:02:33| CRI


Serikali ya mpito ya Mali imesema vikosi vya ulinzi na usalama vya Mali hivi karibuni vilizuia jaribio la mapinduzi ya kijeshi.

Taarifa iliyotolewa na serikali hiyo imesema, baadhi ya wanajeshi walijaribu kufanya mapinduzi ya kijeshi usiku wa tarehe 11 na 12, na kudai kuwa askari hao wanaungwa mkono na nchi za Magharibi.

Serikali ya mpito ya Mali inachunguza na kutafuta wahusika wa jaribio hilo la mapinduzi.