Rais wa China ahutubia ufunguzi wa mkutano wa BRICS
2022-05-19 21:28:09| CRI

Rais Xi Jinping wa China amehutubia ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za BRICS, zinazojumusisha nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Kwenye hotuba yake Rais Xi amesisitiza kuwa, wakati dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali, maendeleo ni kazi ya pamoja ya nchi zinazoibuka kiuchumi na zile zinazoendelea, na kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya nchi hizo ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote uliopita. Ameongeza kuwa, nchi za BRICS zinapaswa kufanya mazungumzo na mawasiliano na nchi nyingine zinazoibuka kiuchumi na zile zinazoendelea, kukuza maelewano na kuaminiana, kuimarisha ushirikiano, na kuongeza maslahi ya pamoja, ili kutoa mchango zaidi kwa kutimiza lengo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi pia ametoa salamu za pongeza kwa kongamano la vyama vya kisiasa, majopo ya washauri bingwa, na mashirika ya kiumma ya BRICS lililofanywa kwa njia ya mtandao.