Rais wa China ahutubia mkutano wa kilele wa kuhimiza biashara duniani
2022-05-19 09:09:41| CRI

Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano wa kilele wa kuhimiza biashara duniani, ambao pia ni mkutano wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Kamati ya Kimataifa ya China ya Kuhimiza Biashara Duniani.

Katika hotuba yake, rais Xi amesisitiza kuwa China haitabadilisha nia yake ya kufungua mlango, na itaendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini humo. Amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita, ikiwemo janga la COVID-19, na watu wa viwanda na biashara wanatarajia zaidi amani, maendeleo, haki na mafanikio ya pamoja. Ametoa mapendekezo manne, ambayo ni kushirikiana ili kushinda janga la COVID-19, kustawisha tena biashara na uwekezaji, kushikilia uvumbuzi na kukamilisha usimamizi wa mambo ya kimataifa.