Mkutano wa uchumi wa Afrika wamalizika kwa kutoa wito wa utaratibu mpya wa kifedha wa kimataifa
2022-05-19 08:35:05| CRI

Mkutano wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi kutoka nchi za Afrika umemalizika kwa kutoa wito wa utaratibu mpya wa kifedha wa kimataifa utaoweza kutimiza mahitaji ya kifedha ya Afrika.

Mkutano huo ulioandaliwa na Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA), ulifanyika mjini Dakar, Senegal kwa njia ya mtandao na moja kwa moja.

Akihutubia mkutano huo, rais wa Senegal Macky Sall amesema, janga la COVID-19 linaloendelea limeonyesha kuwa taasisi zilizopo sasa hazifanyi kazi kwa nchi zinazohitaji msaada wao zaidi. Amewataka wenzi wa maendeleo wa Afrika kujadili upya kanuni za mfumo wa sasa wa pande nyingi kwa kuzingatia mshtuko wa uchumi wa dunia kutokana na janga la COVID-19 na mgogoro wa Russia na Ukraine.