Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za BRICS kufanyika leo
2022-05-19 09:08:49| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za BRICS utafanyika leo kwa njia ya video, na utaendeshwa na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi.

Wang Wenbin amesema, BRICS ni mfumo wenye ushawishi wa kimataifa wa ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea na zinazoibuka kiuchumi, una maana maalum kwa kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo, na unahimiza kufufuka kwa uchumi wa dunia baada ya janga la COVID-19.