China yatoa takwimu mpya za viumbeanuai
2022-05-23 08:44:38| CRI

China imetoa takwimu mpya za kitaifa za spishi za viumbeanuai, ijulikanayo kama Katalogi ya Orodha ya Mwaka 2022 ya Viumbe hai vya China.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Sayansi ya China (CAS), orodha ya mwaka huu imeongeza spishi 10,343 ikilinganishwa na ya mwaka jana, na kufanya jumla ya spishi kuwa 138,293, zikiwa ni pamoja na spishi za wanyama 68,172, spishi za mimea 46,725 na spishi za kuvu 17,173 miongoni mwa nyingine. Afisa wa Kamati ya Viumbeanuai iliyo chini ya CAS, amesema orodha hiyo ya spishi inatoa takwimu ambazo zinanufaisha utafiti wa viumbeanuai, uhifadhi na utungaji sera, na kwamba China ni nchi pekee inayotangaza orodha yake ya sipishi ya viumbeanuai kila mwaka.

Orodha hii imekusanywa kwa pamoja na watafiti kutoka taasisi ya wanyama (Zoolojia), taasisi ya mimea (Botania) na Taasisi ya viumbe vya baharini (Oceanolojia) chini ya CAS pamoja na taasisi nyingine.