Mtoto wa Mama-Na Adam Shafi
2022-05-23 11:05:58| cri

Mtoto wa Mama ni riwaya inayotoa taswira ya maisha ya familia ya mzazi mmoja, Zamda na mtoto wake, Saburi. Wote wamepotelewa, Zamda na mume wake Shauri, na Saburi na baba yake. Hawajui alipo. Hawajui kama yu hai au kafa.

Walipojua, tayari Jalala, mtawala mkuu wa nchi, alikuwa tayari amemhukumu Shauri adhabu ya kifo kwa kunyongwa hadharani. Kabla ya hukumu hiyo kutekelezwa, Shauri tayari kitanzi kimemzunguka rohoni.