Baraza la Afya Duniani lakataa tena mswada kuhusu Taiwan
2022-05-23 21:33:37| cri

Tarehe 23, Mkutano wa 75 wa baraza la Afya Duniani ulifanyika mjini Geneva. Kamati Kuu ya baraza hilo na mkutano huo vimepitisha uamuzi wa kukataa kuwekwa kwenye ajenda ya mkutano mswada uliotolewa na nchi kadhaa kuhusu "kuialika Taiwan kushiriki kwenye mkutano wa baraza hilo kama mwangalizi". Hii imeonesha kuwa kanuni ya kuwepo kwa China moja imekuwa maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

 

Mwakilishi wa China amesema mswada kuhusu Taiwan hauna msingi wa kisheria. Azimio namba 2758 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Azimio namba 25.1 la Baraza la Afya duniani vimeweka msingi wa kisheria kwa Shirika la Afya Duniani WHO kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja. Mswada kuhusu Taiwan hauna msingi wa ukweli wa mambo, na "pengo katika mfumo wa kimataifa wa kuzuia janga la virusi" halikuwepo kabisa.


Baraza la Afya Duniani tayari limefikia hitimisho kuhusu masuala yanayohusiana na Taiwan, na Baraza hilo limekataa kujadili miswada kuhusu Taiwan kwa miaka mingi. Lengo halisi la mamlaka inayoongozwa na Chama cha DPP cha Taiwan ni kutafuta ufarakanishaji kwa kisingizio cha kuzuia janga la virusi. Baadhi ya nchi zinaiunga mkono mamlaka ya Taiwan, lakini hila yao ya kisiasa ya kuiwekea vikwazo China kupitia Taiwan haitashinda kamwe.