Sudan yakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula au hata kuwa mgogoro wa chakula mwaka 2022
2022-05-23 08:53:58| CRI

Wataalamu nchini Sudan wameonya kuwa mwaka huu nchi hiyo inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula au hata kuwa mgogoro wa chakula, na idadi ya watu wanaoathiriwa na njaa inaweza kuongezeka na kufikia milioni 18 ambayo ni asilimia 45 ya jumla ya watu wa nchi hiyo.

Mchumi wa Sudan Bw. Abdul-Khaliq Mahjoub amesema, vyanzo vikuu vitatu vinavyosababisha ukosefu wa chakula nchini Sudan ni pamoja na mgogoro kati ya Russia na Ukraine, sera za uchumi wa ndani na uzalishaji duni wa kilimo.

Amesema, inafahamika kuwa asilimia 90 ya ngano ya Sudan inatoka Russia na Ukraine, na sasa ni vigumu kupata chanzo mbadala. Nchi hiyo inakabiliwa na hatari inayoonekana kwamba haina uwezo wa kununua ngano kwa gharama kubwa.

Hivi sasa bei ya tani moja ya ngano nchini Sudan imezidi dola mia 6 za kimarekani, ambayo imekuwa asilimia 180 juu zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.