Xi Jinping na baba yake
2022-05-24 14:47:54| cri

“Wewe ni kama ng’ombe anayelima kwa bidii, siku zote unawahudumia watu wa China kwa moyo wote. Hii inanitia moyo nijikite katika mambo ya kuwahudumia wananchi.” Xi Jinping aliwahi kumsifu baba yake Xi Zhongxun kwenye barua aliyomwandikia kusherehekea siku ya kuzaliwa. Xi Jinping alisema anatumai kurithi na kuenzi sifa nyingi nzuri kutoka kwa baba yake, na moja ni uaminifu na upendo kwa nchi. 

Xi Zhongxun ni “kiongozi aliyejitokeza kutoka watu wa kawaida”. Aliwahi kusema mara nyingi kuwa yeye ni mtoto wa wakulima, na siku zote anajichukulia kama mmoja wa wafanyakazi wa kawaida. Xi Zhongxun alishuhudia vipindi mbalimbali vya kihistoria vya mapinduzi, ujenzi na mageuzi katika maisha yake. Akishudhudia Maadhimisho ya Miaka 50 tangu Kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Zhongxun alisema: “Kamwe tusisahau kwamba nchi ni watu, na watu ni nchi.”

Tokea Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Rais Xi Jinping alitembelea maeneo yote 14 yenye umaskini uliokithiri, kufanya ziara za ukaguzi na uchunguzi zaidi ya mara 50 kuhusu kazi ya kupunguza umaskini, ili kuhakikisha umaskini unatokomezwa kabisa. Xi Jinping husema, akiwa kiongozi, jukumu lake ni kuwanufaisha wananchi. 

“Sitakuwa na moyo wa ubinafsi, na kubeba majukumu ninayopewa na wananchi.” Huu ndio moyo wa pamoja wa Xi Jinping na baba yake wa  uaminifu na upendo kwa nchi.