Mjumbe wa China atoa mwito wa kuboresha hali ya usalama na kibinadamu nchini Somalia
2022-05-24 09:19:55| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Dai Bing jana alitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi za kuimarisha hali ya usalama na kibinadamu nchini Somalia wakati nchi hiyo ikifanikisha uchaguzi wa rais na wabunge.

Bw. Dai Bing amesema China inatarajia kuwa Somalia itaunda serikali mpya na kutumai kuwa itatumiafursa hii kuharakisha ujenzi wa taifa na kutimiza utulivu na usalama wa muda mrefu mapema iwezekanavyo.

Ameongeza kuwa, amani na utulivu nchini Somalia bado ni masuala yanayokabiliwa na changamoto nyingi, na kusisitiza kuwa jambo muhimu kwa Somalia katika kukabidhi majukumu ya usalama ni kutekeleza mpango wa mpito nchini, kuharakisha uundaji na ujumuishaji wa jeshi lake, na kuboresha uwezo wake wa usalama kwa ufanisi.