Baraza kuu la Umoja wa Mataifa latoa mwito wa kufanya juhudi za kupunguza mgogoro wa usalama wa chakula
2022-05-24 09:16:29| CRI

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limetoa azimio likitaka zifanyike juhudi za kimataifa kupunguza mgogoro wa usalama wa chakula.

Azimio hilo limetoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono haraka nchi zinazoathiriwa na mgogoro wa usalama wa chakula kupitia hatua za uratibu, ikiwa ni pamoja na utoaji wa msaada wa dharura wa chakula, mipango ya chakula, uungaji mkono wa kifedha na kuongeza uzalishaji na aina za mazao ya kilimo.

Wakati huohuo, azimio hilo limetoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa yakiwemo makundi ya G7 na G20 kuweka usalama wa chakula duniani katika nafasi ya mwanzo ya ajenda zao na kuunga mkono juhudi za kimataifa katika kutafuta utatuzi unaofaa wa mgogoro huo.