Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na kamishna mwandamizi wa UM anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu
2022-05-24 09:22:16| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana alikutana na kamishna mwandamizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu Bibi Michelle Bachelet mjini Guangzhou, China.

Wang Yi amemkaribisha Bachelet kwa ziara yake ya kwanza nchini China, akisema hii ni mara ya kwanza kwa China kumkaribisha mwandamizi wa UM anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu baada ya miaka 17, tukio ambalo lina maana ya kihistoria kwa pande zote mbili.

Wang amesema anatarajia ziara ya Bachelet italeta maelewano, kuimarisha ushirikiano na kufafanua mambo. Wang amesisitiza kuwa Chama cha Kikomunisti cha China siku zote kinawapa wananchi kipaumbele, na kuwaongoza Wachina kufuata njia ya ujamaa wenye umaalum wa China inayoendana na hali halisi ya nchi, na kupata mafanikio ya kihistoria katika mageuzi na kufungua mlango, kitendo ambacho kinaungwa mkono sana na watu wa China.

Aidha amefafanua kuwa China siku zote inatoa kipaumbele kwa haki ya uhai na maendeleo, inalinda haki na maslahi halali ya wananchi na kulinda haki za makabila madogo.