Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na ofisa mwandamizi wa UM Michelle Bachelet
2022-05-25 19:05:54| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo amefanya mazungumzo na Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Haki za Binadamu OHCHR Bibi Michelle Bachelet kwa njia ya video.

Kwenye mazungumzo hayo Rais Xi amesema China inapenda kufanya mazungumzo na ushirikiano na pande mbalimbali kwa msingi wa usawa na kuheshimiana, kupanua maelewano, kupunguza tofauti, kufundishana na kupata maendeleo kwa pamoja, ili kuhimiza mambo ya kimataifa ya haki za binadamu. Pia amesisitiza kuwa la muhimu zaidi kwa sasa ni kushughulikia vizuri mambo manne, yakiwa ni kushikilia kutoa kipaumbele kwa wananchi, kuheshimu njia za nchi mbalimbali za kuendeleza haki za binadamu, kuratibu haki mbalimbali za binadamu, na kuimarisha usimamizi wa haki za binadamu duniani.
Bibi Bachelet amesema OHCHR inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na China, ili kufanya juhudi za pamoja kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya haki za binadamu duniani.