Kampuni ya China yazindua mfuko wa maendeleo kusaidia jamii nchini Sierra Leone
2022-05-25 10:38:52| CRI

Kampuni moja ya uchimbaji madini ya China jana ilitangaza kuzindua mfuko wa maendeleo ya kijamii ili kusaidia kuhimiza maendeleo ya jamii nchini Sierra Leone.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na kampuni ya Leone Rock Metal, kampuni hiyo itachukua asilimia 1 ya mapato yake ya kila mwaka kwenye mfuko huo ili kuunga mkono jamii za eneo la Tonkolili, mkoa wa Kaskazini nchini Sierra Leone, ilipo kampuni hiyo.

Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Zhao Ting amesema kampuni hiyo ya China siku zote inajitolea kwenye ajenda ya kuendeleza viwanda huku ikisaidia katika maendeleo ya jamii za wenyeji.

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio amesema hatua iliyochukuliwa na kampuni ya China ni muhimu kwa maendeleo ya jamii.