Waziri mkuu wa China asisitiza utekelezaji wa sera za kutuliza uchumi
2022-05-26 10:51:21| CRI

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alisisitiza umuhimu wa kutekeleza sera za kutuliza uchumi na kuunga mkono masoko, ajira na maisha ya watu.

Bw. Li Keqiang aliyasema hayo kwenye mkutano wa baraza la serikali la China, na kuhimiza juhudi za kuhakikisha uchumi wa taifa unaendeshwa kwa kiwango kinachofaa.

Amesema kuwa, hatua mbalimbali zenye ufanisi zimetekelezwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zisizotarajiwa ambazo zimeibuka mwaka huu. Amesisitiza kuwa, maendeleo ni jambo muhimu katika kutatua masuala yote ya China, ni lazima kutekeleza wazo la maendeleo mapya, kusawazisha kwa ufanisi udhibiti wa janga la COVID-19 na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na kutoa kipaumbele katika kutuliza ongezeko la uchumi.