Mabadiliko ya hali ya hewa yana kasi zaidi kuliko ilivyotabiriwa
2022-05-27 09:17:03| CRI

Utafiti mpya uliotolewa jana umeonyesha kuwa, mchakato wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani una kasi zaidi kuliko ulivyotarajiwa na hatua za haraka zinahitajika ili kupunguza uharibifu.

Kwenye utafiti huo uliotolewa na jarida la Nature Claimate Change, watafiti kutoka taasisi ya sayansi ya Weizmann WIS nchini Israel, idara ya bahari na anga ya Marekani NOAA na Chuo kikuu cha teknolojia cha Massachusetts MIT, wanasema dhoruba za majira ya baridi zitaongezeka kwa kiasi kikubwa katika sehemu ya kusini ya dunia.

Kulingana na muundo wa mifano ya hali ya hewa na uchunguzi wa sasa wa dhoroba, timu hiyo imegundua kwamba ongezeko la dhoruba zilizosababishwa na shughuli za binadamu limeshafikia kiwango kilichotabiriwa kutokea mwaka 2080.