Mjumbe wa China ailaumu Marekani kwa kushindwa ikiwa kama kiongozi anayeshughulikia vikwazo vya Sudan Kusini
2022-05-27 09:14:21| CRI

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun jana aliilaumu Marekani kwa kushindwa kutimiza wajibu wake ikiwa kama kiongozi wa Baraza la Usalama anayeshughulikia vikwazo vya Sudan Kusini.

Wajibu wa kiongozi anayeshughulikia vikwazo ni kusaidia Baraza la Usalama kutoa azimio litakalokuwa na upeo wa makubaliano, na sio kusisitiza mtazamo wake binafsi kwenye azimio hilo. Amebaninisha kuwa Marekani haikusikiliza kwa makini na kutumia maoni ya busara, haikuonesha usawa na ujumuishi anaopaswa kuwa nao kiongozi, na imeshindwa kabisa kutilia maanani wasiwasi wa pande zote wakati iliporekebisha azimio.

Idadi kubwa ya wajumbe, wakiwemo wa nchi zote za Afrika wa Baraza la Usalama, wamevunja ukimya wao kutokana rasimu ya azimio iliyotowekwa na Marekani. Hata hivyo Marekani bado imelazimisha azimio hilo ambalo halikuridhiwa na wengi, kupigiwa kura.