China itaendelea kupambama kithabiti na janga la Covid-19
2022-05-31 09:07:04| CRI

Wakati China inaendelea na sera yake madhubiti ya kupambana na Covid-19,

baadhi ya watu wanaweza kudhani sera thabiti ya China m haiendani na uhalisia, hasa kutokana na  changamoto za maambukiza ya virusi vya Covid-19 aina ya Omicron. Lakini ni uamuzi wa kila nchi kuamua sera inayitaka kufuata kupambana na janga la Covid-19. Sera yenye unyumbufu ni sera ya afya ya umma ambayo imetekelezwa sio tu na China bara bali pia imetekelezwa kwa viwango tofauti katika maeneo mengine matatu ya China (Taiwan, na mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Macao). Cha kusikitisha ni kuwa, viongozi wa afya wa Taiwan waliacha sera hiyo hivi karibuni, na kisiwa hicho sasa kinakabiliwa na matokeo mabaya ya kukabiliana na ongezeko kubwa la maambukizi ya ndani, na hata vifo. Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha California,  Los Angeles mwezi uliopita, asilimia 30 ya watu waliotibiwa COVID-19 waliendelea kuwa na dalili za ugonjwa huo ziliozoendelea kwa muda mrefu m kama, hali inayoweza kuweka shinikizo kubwa kwa mifumo ya afya ya umma duniani kote kwa miongo kadhaa. Mbali na China nchi nyingine kama vile Australia, Singapore na Korea Kusini zilikuwa na sera ya sifuri ya COVID-19 hadi hivi karibuni, lakini ziliamua ghafla kubadilisha sera hiyo, hasa kwa sababu za kiuchumi.

Tofauti na nchi hizo, China ni nchi yenye idadi kubwa sana ya watu (bilioni 1.4), na bado mfumo wake wa afya uko kwenye mchakato wa kuimarishwa, haiwezi  kukabiliana na shinikizo kubwa 

kuna uelewa mbaya kwa nchi za magharibi kuhusu sera ya kupambama na Covid-19, zikifikiri kuwa sera hiyo maana yake ni kutokuwa na virusi kabisa.

Mkuu wa jopo la wataalam la kupambana na Covid-19 katika kamati ya afya ya taifa (wizara ya afya) aliweka wazi mwanzoni mwa mwaka huu, kwamba sera yenye unyumbufu ya virusi vya COVID kuwa sifuri, maana yake ni kuhakikisha kuwa janga hili nchini China lisifikie hatua ya kutodhibitika.