Xi Jinping asema China inapenda kuhimiza uhusiano wake na Zambia uendelee kwa kiwango cha juu na kupanuka zaidi
2022-06-01 08:54:35| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema China inatilia maanani sana uhusiano wake na Zambia, na inapenda kushirikiana nayo katika kuhimiza uhusiano wa pande mbili uendelee kwa kiwango cha juu na kupanuka zaidi. Hayo ameyasema jana wakati alipoongea kwa simu na mwenzake wa Zambia Hakainde Hichilema.

Kwenye mazungumzo yao, Xi amebainisha kuwa China na Zambia ni wenzi wa siku zote. Katika mwaka uliopita, thamani ya biashara kati ya nchi mbili imefikia kiwango cha juu zaidi, Zambia imekuwa nchi ya Afrika inayoivutia zaidi China kuwekeza moja kwa moja.

Xi amesisitiza kuwa China na Zambia zinapaswa kuungana mkono masuala yanayohusu maslahi makuu ya nchi mbili, kuimarisha mawasiliano ya vyama, kubadilishana uzoefu juu ya utawala wa nchi, kutekeleza kikamilifu “miradi tisa” iliyotolewa na mukutano wa nane wa mawaziri wa FOCAC wa mwaka 2021, kuhamasisha bidhaa nyingi zaidi za Zambia hasa bidhaa za kilimo ziingie kwenye soko la China, na kuimarisha ushirikiano katika kupambana na virusi vya Corona.

Wakati huohuo, rais Hakainde Hichilema ameisifu China kwa kuisaidia Zambia kujenga Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Kenneth Kaunda.