Xi Jinping atoa salamu za pongezi kwa rais Mohamud wa Somalia
2022-06-01 11:42:44| cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa Bw. Hassan Sheikh Mohamud kutokana na kuchaguliwa kwake tena kuwa rais wa Somalia.

Katika salamu zake, rais Xi anasema upo urafiki wa muda mrefu kati ya China na Somalia, nchi ambazo siku zote zinaungana mkono kidhabiti katika masuala yanayohusu maslahi kuu ya pande hizo mbili. Rais Xi anaeleza kuzingatia sana kukuza uhusiano kati ya China na Somalia, angependa kufanya juhudi pamoja na rais Mohamud, ili kusukuma mbele ushirikiano wa nchi hizo mbili katika fani mbalimbali na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.