Balozi wa Mauritius: Mauritius yapenda kuwa daraja kati ya Afrika na China
2022-06-02 10:36:24| CRI

Karibu msikilizaji katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Miongoni mwa mambo tuliyokuandalia katika kipindi cha leo ni habari mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, ripoti inayohusu Mauritius inavyotaka kuwa daraja kati ya Afrika na China, lakini pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi, ambayo yatamhusu kijana wa Kichina nchini Kenya ambaye anawasaidia watoto kutoka mtaa wa mabanda wa Mathare kuendelea kuhudhuria shuleni kupitia mpango wa kupatia chakula unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la China (NGO).