TASAF yaziondoa kaya zaidi ya laki moja kwenye umaskini uliokithiri
2022-06-02 09:55:01| CRI

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) ulioanzishwa na serikali mwaka 2000 kwa ajili ya kufanya juhudi za kupunguza umaskini jana ulisema kaya zaidi ya 105,000 zimeondokana na umaskini uliokithiri.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga amesema, kaya maskini 105,382 zimeboresha zaidi maisha yao kiuchumi kwenye sekta mbalimbali. Mafanikio ya TASAF yaliyopatikana hadi sasa yanatokana na ahadi ya serikali katika kuhakikisha maendeleo shirikishi kwa wananchi wake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameisifu TASAF kwa kuboresha maisha ya watu.