Rwanda yakaribisha uamuzi wa DRC wa kuwaachia huru askari wake
2022-06-03 09:17:52| CRI

Msemaji wa serikali ya Rwanda jana alisema Rwanda inakaribisha uamuzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wa kuwaachia huru askari wake wawili waliokamatwa mwezi uliopita.

Rwanda imesema askari hao wawili walitekwa nyara walipokuwa wakifanya doria kwenye mpaka  na kushutumiwa kushirikiana na waasi wa jeshi la FDLR kwa kurusha roketi kwenye ardhi ya DRC na kusababisha majeruhi ya raia.

Vyombo vya habari Jumatano viliripoti kuwa rais Felix Tshisekedi wa DRC amekubali kuwaachia askari hao wawili kama sehemu ya jitihada za kupunguza hali ya wasiwasi.