Mwenyekiti wa AU Macky Sall akutana na rais Putin wa Russia
2022-06-03 09:17:16| CRI

Kutokana na mwaliko wa rais wa Russia Vladimir Putin, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) ambaye pia ni Rais wa Senegal Macky Sall jana Alhamis aliondoka Dakar kuelekea Moscow.

Akiambatana na mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat, leo rais Sall atakutana na mwenyeji wake Putin mjini Sochi.

Ziara hiyo inalenga kuishawishi Russia kuachilia nafaka na mbolea zilizozuiwa kusambazwa, kitendo ambacho kimeathiri zaidi hasa nchi za Afrika, na pia kupunguza mzozo kati ya Ukraine na Russia.

Baada ya kuondoka Sochi, rais Sall ataelekea Accra nchini Ghana kuhudhuria mkutano wa kilele wa ECOWAS Jumamosi utakaojadili hali ya Mali, Guinea na Burkina Faso.