Wafanyakazi wengi Wamarekani wenye asili ya Afrika waondoka katika ikulu ya white house
2022-06-03 09:19:35| CRI

Zaidi ya wafanyakazi 20 ambao ni Wamarekani wenye asili ya Afrika wameripotiwa kuondoka katika ikulu ya white house ya Joe Biden kuanzia mwaka jana, huku baadhi ya watu wakiwapa jina la “Blaxit”.

Wakati baadhi yao wakiondoka kwa nia njema ili kujiendeleza zaidi kiajira au kutafuta fursa za elimu, wengine wamehusishwa kuondoka kutokana na kukosa fursa na kutoa maamuzi. Akiongea na chombo cha habari mmoja wa waliondoka alisema wapo ikulu wakifanya kazi nyingi lakini hawapati fursa ya kutoa maamuzi, na kwa wao wanaona hakuna mwelekeo wa kuwa watoa maamuzi.

Afisa mwengine alisema kwamba wamepeleka watu weusi kuanza kazi bila kuanzisha miundombinu ya kuwadumisha au kuwasaidia kupata mafanikio, na kuhoji kwamba kama hakuna miundo mbinu ya kuwafanya wafanikiwe, inakuwa ni sawa na mtu asiyeonekana mahali alipo kuliko akiondoka mahali hapo.