WHO: Idadi ya vifo vinavyotokana na COVID-19 barani Afrika yatarajiwa kupungua kwa asilimia 94 mwaka 2022
2022-06-03 09:18:26| CRI


Shirika la Afya Duniani WHO jana lilinukuu uchambuzi mpya unaosema kwamba, idadi ya vifo vinavyotokana na COVID-19 barani Afrika inatarajiwa kupungua kwa asilimia zaidi ya 94 mwaka 2022 kuliko mwaka 2021 ambao ulikuwa na vifo vingi zaidi vya maambukizi hayo.

Ofisa wa kikanda wa WHO barani Afrika ametoa taarifa akisema, uchambuzi huo uliotolewa kwenye jarida la The Lancet Global Health, unasema kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2022, kutakuwa na vifo vya watu karibu elfu 23 kama virusi vinavyobadilika sasa na mienendo ya maambukizi vitaendelea mara kwa mara, kwani kesi za maambukizi zinakadiriwa kupungua kwa zaidi ya robo katika mwaka huu.

Kwa mujibu wa uchambuzi huo, nchi za Afrika zimeripoti vifo 113,102 katika mwaka 2021 kwa njia rasmi, lakini karibu theluthi moja ya vifo haikuonekana na idadi halisi ya vifo ilikuwa karibu laki 3.5.