Chombo cha anga za juu cha Shenzhou-14 kilichobeba wanaanga watatu charushwa huko Jiuquan, China
2022-06-05 11:56:20| CRI

Chombo cha anga za juu cha Shenzhou-14 cha China kilichobeba wanaanga watatu kimerushwa kwa mafanikio kwa kutumia roketi ya Long March-2F Y14 tarehe 5 mwezi wa Juni kutoka kwenye kituo cha kurushia vyombo vya anga za juu cha Jiuquan, kaskazini magharibi mwa China.

Kwa mujibu wa mpango, baada ya kufika katika obiti, chombo hicho kitatia nanga kwenye moduli kuu ya Tianhe ya kituo cha anga za juu cha China. Wanaanga watatu katika chombo hicho wataishi na kufanya kazi kwa miezi sita kituoni humo, ambapo watafanya kazi mbalimbali za kukamilisha ujenzi wa kituo hicho pamoja na majaribio ya kisayansi na kiteknolojia katika anga za juu.