Riwaya ya Maisha ya Hatari- iliyoandikwa na H.R Ole Kulet
2022-06-06 10:08:47| cri

Riwaya hii ni yenye mafunzo maalum kuhusu maisha yetu ya kila siku.

Muhusika Jusufu Kabita ni kijana ambaye hakufanikiwa kupata elimu ya msingi maishani mwake. Ingawaje, alijikakamua kwa kuwafuga mbwa na kuwauzia polisi. Alifua dafu kwa sababu ya bidii yake lakini akapatana na kipusa ambaye alimwingiza kwenye mtego kisha mambo yakamwendea segemnege.