China yarusha chombo cha anga za juu kumalizia ujenzi wa kituo cha anga za juu cha China
2022-06-06 08:48:25| CRI

China jana imerusha chombo cha anga za juu cha Shenzhou-14 kilichobeba wanaanga watatu watakaomalizia ujenzi wa kituo cha anga za juu cha China katika jukumu litakalochukua miezi sita.

Wanaanga hao watashirikiana na timu iliyoko duniani kumaliza kuunga na ujenzi wa kituo cha anga za juu cha Tiangong, wakikiendeleza kutoka muundo wake wa jengo moja na kukibadilisha kuwa maabara ya kitaifa ya anga za juu yenye maeneo matatu: chombo kikuu cha Tianhe na maabara mbili za Wentian na Mengtian.

Hii ni safari ya 23 ya anga za juu tangu kuidhinishwa na kuanzishwa kwa mradi wa taifa wa anga za juu, na pia ni mradi wa tatu unaohusisha kupeleka wanaanga katika kituo cha anga za juu cha China.