Tume ya uchaguzi nchini Kenya yapitisha majina ya wagombea urais katika uchaguzi wa mwezi Agosti
2022-06-06 08:50:02| CRI

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) imewapitisha wagombea urais wawili na wagombea wenza wao katika uchaguzi wa nafasi hiyo utakaofanyika Agosti 9 mwaka huu.

Naibu rais wa Kenya William Ruto anayegombea nafasi hiyo kupitia muungano wa Kenya Kwanza na mgombea mwenza wake Rigathi Gachaguwa walikuwa wa kwanza kupitishwa kugombea nafasi hiyo baada ya kutimiza vigezo vinavyotakiwa.

Mgombea mwingine aliyepitishwa na Tume hiyo ni Raila Odinga anayegombea nafasi hiyo chini ya muungano wa Azimio la Umoja linalojumuisha vyama vya siasa zaidi ya 20 na mgombea mwenza wake Martha Karua.