Jeshi la Somalia lamuua kamanda mwandamizi wa al-Shabab
2022-06-06 08:49:46| CRI

Jeshi la Somalia (SNA) limemuua kamanda mwandamizi wa kundi la al-Shabab Jumamosi katika operesheni yake iliyofanyika kusini magharibi mwa nchi hiyo

Makamanda wa jeshi walioongoza operesheni hiyo wameambia Televisheni ya Taifa ya Somalia kwamba, Mohamed Nur Ga'al, anayejulikana pia kama Sheikh Al-Sima, ameuawa karibu na El-unit, mjini Tiyeglow katika eneo la Bakool.

Habari zinasema Nur alikuwa kiongozi mwandamizi wa al-Shabab aliyehusika na mashambulizi mengi ya kigaidi katika maeneo ya Bay na Bakool.

Vikosi vya usalama vya Somalia, vikisaidiwa na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika, vimeongeza mashambulizi dhidi ya kundi la al-Shabab, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuleta utulivu nchini humo.